Mkoa wa Geita umetajwa kuwa ni mkoa ambao una matumizi makubwa ya zebaki(mecury) ambayo inatumika kunasa dhahabu wakati wa uchakatuaji hivyo kufanya matumizi ya zebaki kufiki tani 18-27 ukilinganisha na takwimu zilizofanywa mwaka 2020 ambapo matumizi ya zebaki yalikuwa tani 12-27.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo alipokuwa katika semina ya kudhibiti matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo Injinia Dokta Befrina Igulu mratibu wa mradi kutoka baraza la taifa la usimamizi na uhifadhi wa mazingira (NEMC)alisema takwimu hizi zimeongezeka kutokana na ongezeko kubwa la wachimbaji wadogo.
Befrina aliongeza kuwa NEMC imejipanga kuweka mikakati na kutoa elimu ya kudhibiti matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo ikiwa pamoja na kuimarisha mifumo za kitaasisi iweye kuwa na udhibiti imara.
Nae meneja wa mradi huo Evance Lubala alitoa wito kwa wachimbaji wadogo kuwa wakubaliane na mabadiliko yanayokuja ya kuachana kabisa na matumizi ya yebaki kwa ina athari kubwa kwao.