Ni Waziri Rajabu Salum ambae ni katibu binafsi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambae kupitia ukurasa wake wale mtandao wa kijamii ‘instagram’ ameweka picha akiwa na Godfrey Magilla huku akiambatanisha ujumbe unaolenga kijana anaepambania Kombe katika harakati za Maisha.
Godfrey Magila ni Mmiliki wa Kampuni ya Magilatech ambayo inahusika katika utengenezaji na ulinzi wa mifumo ya kidigital ,imejikita zaidi kwenye utengezaji wa Mifumo ya Malipo, Mawasiliano na Elimu na kwenye Upande wa Ulinzi wa Mifumo imekuwa ikitoa huduma ya kulinda mifumo kwa kuidukua kabla ya wadukuzi nakuziba njia ndani na nje ya nchi.
Nukuu……
‘Mdogo wangu @godfreymagila akaniuliza kaka mbona huonekani kabisa umepotea Kabisa?
‘Nikamwambia tunakwepa kukutana na watu si kwasababu sipendi Hapana ila tunaogopa kupiga shoti, dunia imejaa wapiga shoti kuliko wazimaji wa shoti na tumefikia hatua hujui nani ni nani watu wamekuwa na tabia za kishetani’- Waziri Rajabu Salum
‘Sasa kuepukana na kupigwa shoti wahi nyumbani kwako ukakae na watoto wako…. Maana Vijana tumefikia hatua kumuharibia mtu maisha yake na heshima yake basi mtu anajisikia ufahari na şifa’- Waziri Rajabu Salum
‘Ila Mungu nae fundi huwapiga wapiga shoti kwa jambo moja kubwa sana, Mungu huwa huwainui kwenye maisha yaani kazi yako utakuwa kupiga watu shoti tu na upo hapohapo ukiamini una taarifa za watu wote ila unakosa taarifa zako za kukufanya utoke hapo ulipo’- Waziri Rajabu Salum