Wakiwa bado hawajasahau tetemeko lililotokea kwenye wiki mbili zilizopita, raia wa Nepal wameingiwa na hofu kubwa baada ya kukumbwa na tetemeko lingine kubwa, tetemeko la kwanza lililotokea April 25 lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 8,000 na inasemekana kuwa tetemeko hilo lilianzia katika mji wa Namche Bazar karibu na milima ya Evarest.
Inasemekana tetemeko hilo limefikia kipimo cha magnitude 7.3 ikilinganishwa na awali ambalo lilifikia kipimo cha 7.8 na tayari watu 29 wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine zaidi ya 1000 wakijeruhiwa vibaya.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyezahapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahaukusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video yaAyoTVikufikie.