Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameapa kuendelea na Vita dhidi ya Wapiganaji wa Hamas huko Gaza, huku mgogoro huo ukiingia mwaka wake wa 12, akizungumza kwenye Mkutano wa kila wiki wa Viongozi wa Serikali, Netanyahu alisema kuwa “Israel inazungukwa na itikadi katili inayoongozwa na mhimili wa uovu wa Iran.”
Katika Shambulio la hivi karibuni, Watu watatu wa Israeli waliuawa na mwanamgambo aliyefyatua Risasi kwenye Daraja la Allenby linalounganisha Ukingo wa Magharibi na Jordan, huku Vikosi vya Usalama vya Israeli vikimuuwa mshambuliaji huyo.
Aidha huko Gaza, mashambulizi ya anga ya Israeli yamewauwa Watu watano, wakiwemo Wanawake wawili, Watoto wawili, na Afisa wa Msalaba Mwekundu wa eneo hilo.
Netanyahu ameahidi kuendelea na Operesheni hadi Hamas itakaposambaratishwa na Mateka wote wa Israel kurejeshwa.
Serikali ya Jordan inachunguza tukio hilo huku ikiendelea kukosoa Sera za Israel dhidi ya Wapalestina, Pia maandamano makubwa yameendelea Nchini Israel, Wananchi wakimkosoa Netanyahu kwa kushindwa kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kushughulikia suala la mateka waliotekwa na Hamas.