Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelionya kundi la Hamas dhidi ya kuendeleza mashambulizi ya roketi kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano.
Katika hotuba yake saa chache baada ya kuanza kutekelezwa kwa makubaliano hayo, Netanyahu amesema Hamas itajidanganya iwapo itafikiria Israel itavumilia maroketi inayorusha.
Netanyahu amesema wako tayari kujibu kwa nguvu zote uchokozi wa aina yoyote dhidi ya watu walio karibu na Gaza na katika eneo lolote lile la Israel. Israel na Hamas wameshambuliana kwa siku 11, hivi vikiwa vita vyao vya nne tangu kundi hilo la wanamgambo wa kiislamu lilipochukua madaraka mjini Gaza kutoka kwa vikosi vya Palestina mwaka 2007.
MTOTO JASIRI ANATANGAZA DW, AWASHANGAZA WENGI, ANA UWEZO WA AJABU, AJIZOLEA UMAARUFU MKUBWA DUNIANI