Serikali ya Israel ilitayarisha pendekezo la kuanzisha mazungumzo mapya na kundi la Palestina Hamas kwa ajili ya kuachiliwa kwa mateka wa Israel katika Ukanda wa Gaza lakini Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alikataa ombi hilo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.
Idhaa ya 13 ya Israel iliripoti kuwa mawaziri wa Israel ambao hawakutajwa majina walielezea mfumo mkuu wa makubaliano katika siku za hivi karibuni yenye lengo la kuachiliwa kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas.
Mazungumzo yalitarajiwa kuendelea kupitia mpatanishi ambaye hakutajwa jina, lakini Netanyahu aliripotiwa kukataa hatua hiyo.
Uamuzi wa kukataa pendekezo hilo, kama ilivyoonyeshwa na idhaa, ulifanywa bila kuratibu na mawaziri wa vita Benny Gantz na Gadi Eisenkot.
Channel 13 pia iliripoti taarifa kutoka kwa maafisa wa kisiasa ambao hawakutajwa wakidai kuwa Netanyahu alikuwa anazuia juhudi za kufikia makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka.
Israel inadai kuwa Hamas imekuwa ikiwashikilia Waisraeli 136 huko Gaza tangu Oktoba 7, huku Hamas ikidai kusitishwa kwa mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa wafungwa wa Kipalestina kutoka magereza ya Israel kwa kubadilishana na kuwaachilia wafungwa wa Israel chini ya ulinzi wake.