Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaongeza muda wa vita huko Gaza ili kusalia madarakani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyad Al Maliki amesema.
Aliyasema hayo wakati wa mkutano na Balozi wa Afrika Kusini Sean Benfeldt katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje huko Ramallah, shirika la habari la Palestina WAFA liliripoti.
“Netanyahu hana nia ya kusitisha mapigano. Kinyume chake, anataka kurefusha vita kwa muda mrefu iwezekanavyo ili kusalia madarakani,” alisema Al Maliki.
tazama pia..