Serikali imeendelea na msimamo wake wa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, baada ya Rais Magufuli kuondoa safari za nje, mamilioni ya pesa kuokolewa katika uzinduzi wa Bunge sasa imepiga marufuku uchapishaji wa kadi za sikukuu ya Christmas na mwaka mpya.
Katika taarifa yake Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Christmas na mwaka mpya kwa gharama za Serikali mwaka huu.
Balozi Sefue ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo afanye kwa gharama zake mwenyewe.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa imesema fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji wa uchapishaji wa kadi hizo zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, idara na Taasisi za umma zinadaiwa na wananchi waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine.
Taarifa hiyo ilisomeka hivi
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE