Inaonekana kama Newcastle wako tayari kuachana na harakati zao za kumtafuta mlinzi wa Crystal Palace Marc Guehi, huku klabu hiyo ikionekana kuchoshwa na mazungumzo na Palace.
Newcastle imekataliwa ofa nyingi za kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 katika wiki za hivi karibuni, na mara ya mwisho kukataliwa kwa £60m pamoja na £5m.
Newcastle ilitoa £65m + £5m kama nyongeza kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza lakini mmiliki wa Palace Steve Parish bado hajakubali na muda unakwenda haraka katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Guehi amekuwa akipewa kipaumbele katika klabu ya St James Park lakini klabu hiyo imeona maombi mengi yakikataliwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake.