Ufaulu katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne umeongezeka kwa asilimia 10, chini kidogo ya viwango vya Matokeo Makubwa Sasa (BRN), lakini shule za Serikali za vipaji maalumu, kongwe na za seminari zimeendelea kuporomoka.
Katika matokeo hayo, Shule ya Sekondari ya Kaizirege ya mkoani Kagera, iliyoanzishwa mwaka 2010, ndiyo imekuwa kinara ikiwa ni mwendelezo wa mafanikio baada ya mwaka jana kushika nafasi hiyo lakini kwa upande wa shule zenye watahiniwa chini ya 40. Shule iliyoshika mkia ni Manolo iliyopo Tanga, mkoa ambao umetoa shule tano miongoni mwa shule zilizoshika nafasi 10 za mwisho.
Matokeo hayo ni ya kwanza tangu kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa upangaji wa Wastani kwa Kutumia Pointi (GPA) ambao unaonyesha shule zote 10 za kwanza ni za binafsi.
Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde alisema waliofaulu mtihani huo ni wanafunzi 196,805 sawa na asilimia 68.33 ya watahiniwa 288,247 waliofanya mtihani huo, ikilinganishwa na 235,227, sawa na asilimia 58.25 ya waliofaulu mwaka 2013.
Dk Msonde alisema wavulana waliofaulu ni 106,960 sawa na asilimia 69.85 na wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61.
MWANANCHI
Baada ya Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kuteleza na kuanguka katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Harare, watu wengi duniani wamechukulia kitendo cha kuanguka kwa rais huyo kama staili ya kutembea wakiwa na lengo la kumdhihaki.
Katika nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya watu wamekuwa wakitembea kama vile wanataka kuanguka wakimuigiza Rais Mugabe. Rais Mugabe ambaye ameiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1980, alizaliwa Februari 21, 1924, ambapo mwezi huu atatimiza umri wa miaka 91.
Picha mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha Mugabe akishiriki shughuli mbalimbali, lakini kwa stahili kama alivyoanguka uwanja wa ndege.
Kutokana na picha zilizotengenezwa kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, rais huyo aliagiza picha hizo zifutwe kwakuwa hazina maana.
Baadhi ya picha za Mugabe kwenye mitandao ya kijamii, zinaonekana akikimbizwa na polisi, nyingine akiteleza kwenye barafu na akishangilia mchezo wa kriketi uwanjani.
Moja ya picha iliyoonekana kuwavutia watu wengi ni ile iliyotengenezwa na kuwekwa kwenye moja ya picha Hussein Bolt akiwa anachomoka kwenye mbio za mita 100, huku akiwa sambasamba na mkimbiaji huyo maarufu duniani.
MWANANCHI
Zaidi ya Sh720 bilioni zitatumika kuanika ‘uozo’ wakati wa mchakato wa uandikishaji wapiga kura, kura ya maoni na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es Salaam jana, Meneja Mradi wa Kamati ya Uangalizi wa Chaguzi Tanzania (TEMCO), Dk Benson Bana, alisema kuwa fedha hizo zimetolewa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kuwezesha mpango huo kufanikiwa.
Alisema kuwa kwa mara ya kwanza kamati hiyo, pia itaangalia mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa, utakaojumuisha wagombea urais, ubunge, ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Udiwani.
Baada ya kumalizika kwa hatua hiyo, TEMCO itaandika ripoti ikatakayoweka wazi mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wanasiasa kuteua na kushinda nafasi wanazogombea ikiwamo kununua kura.
“Watazamaji wa uchaguzi watakuwa makini kuangalia mifumo ya kisheria na kitaasisi, uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa, uthabiti wa tume za uchaguzi, utekelezaji wa Sheria ya gharama za Uchaguzi na uteuzi wa wagombea unafanywa na tume za uchaguzi:- Dk Bana.
Aliongeza: “Tunafuatilia ili wananchi wa kawaida wawe na imani na mfumo wa uchaguzi katika nchi yao. Uchaguzi wa mwaka 2000 watu wengine walikuwa wanaogopa kusema sisi tulitokea tukasema hakukuwa na uchaguzi bali uchafuzi na tulifikiri wangetufukuza hawakufanya hivyo.”
Dk Bana alisema zoezi hilo lililofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), litasimamiwa na watazamaji wa muda mrefu 180 watakao angalia zoezi la uandikishaji wapiga kura litakaloanza Februari mwaka huu.
MWANANCHI
Shirika la viwango nchini TBS limepiga marufuku usambazaji wamabati kutoka kampuni ya Uni Metal baada ya kudhibitishwa kuwa hayakidhi vigezo.
Sambambana kuzuiwa kuingia sokoni, TBS imefungia ghala linatumika kuhifadhi mabati hayo yanayoingizwa nchini kutoka India.
Ofisa viwango wa TBS Cyrin Kimario alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kupimwa kwa sampuli ya mabati hayo na kubainika kuwa hayajakidhi viwango licha ya kuwa na nyaraka zinazothibitisha kukaguliwa na wakala aliyekuwa India.
“Pamoja na kukosa viwango vinginevya ubora haya mabatihayana chapa ya kiwanda yanapotengenezwa” :Kimario
NIPASHE
Hali ya wasiwasi imetanda eneo la Amboni jijini Tanga, baada ya mapambano ya risasi kurindima huku askari mmoja wa Jeshi la Wananchi nchini (JWTZ) akipigwa risasi ya tumboni na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo lakini baadaye alifariki dunia.
Mapambano hayo yanadaiwa kudumu zaidi ya saa 48 kuanzia juzi saa 5 asubuhi kwenye maeneo ya maporomoko ya Mikocheni, kijiji cha Amboni umbali wa kilometa 10 kutoka mjini Tanga.
Kamishna wa Operesheni ya Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Paul Chagonja, alithibitisha kujeruhiwa kwa askari polisi watatu, wanajeshi wa JWTZ wawili na mmoja aliyefariki, majeruhi wamelazwa katika hospitali ya mkoa Bombo.
Hata hivyo, alisema askari wanaendelea na operesheni ya kuwatafuta watu hao wanaodaiwa kujificha kwenye mapango ya Amboni.
Alisema mpaka sasa wameshakamatwa watu watatu wakiwa na silaha za jadi ikiwemo mishale, pinde na mikuki.
HABARILEO
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limewakana askari mgambo walioko stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ambao wanadaiwa kugeuka kero kwa kamatakamata na kuomba rushwa watu wenye baiskeli.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda alisema hayo wakati akitoa ufafanuzi wa sakata hilo kwa waandishi wa habari baada ya meneja wa stendi hiyo, Cornery Masawe kutamka askari mgambo hao wamewekwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora Mjini.
Kaganda alisema mgambo hao hawahusiki na ofisi yake wala Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wanawajibika moja kwa moja na halmashauri ya Manispaa Tabora, hivyo aulizwe Mkurugenzi Mtendaji.
Alibainisha kuwa endapo mgambo hao wangekuwa wameagizwa na ofisi ya OCD, hapo angetoa ufafanuzi wake lakini hana cha kusema kutokana na mgambo kutowatambua kuwajibika kwake.
Meneja wa stendi ya mabasi yaendayo mikoani mkoani Tabora, Cornery Masawe kwa mara nyingine alisema mgambo hao hana majibu lakini akaomba aulizwe Kamanda wa Polisi Wilaya ya Tabora Mjini, Benjamini Kuzaga.
Kamanda wa Polisi Tabora Mjini, Benjamini Kuzaga ambaye alipoelezwa juu ya mgambo hao, kwanza alishangaa na kusema hana majibu na msemaji ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kaganda.
Mgambo pamoja na meneja wa stendi hiyo wamelalamikiwa na wananchi wakidaiwa wanapokamatwa na baiskeli zao hata kama hawaendeshi ndani ya stendi hiyo hutozwa faini Sh 20,000, 15,000 au 10,000 lakini
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook