MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameitaka Serikali kuacha siasa kwenye masuala ya kiuchumi, ukiwamo mgogoro kati ya Tanzania na Kenya kuhusu sekta ta utalii.
Akifungua kikao cha Baraza la Uongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Arusha jana, Mbowe aliwataka viongozi Serikali kutumia busara kushughulikia mgogoro huo ulioibuka baada ya Kenya kuzuia magari yenye usajili wa Tanzania kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
“Asilimia 40 ya watalii zaidi ya milioni moja wanaokuja Tanzania kila mwaka, hupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta,”
“Hatustahili kugombana nao, bali tunapaswa kutafuta namna bora ya kushirikiana. Tuna uwezo wa kuchagua marafiki, lakini kamwe hatuwezi kuchagua majirani. Hawa (Kenya) ni wenzetu, tutaendelea kuwa nao pamoja maisha yote.
“Tutunge sera nzuri ya usafiri wa anga na kuvutia kampuni kubwa za ndege kuja kuwekeza nchini kwa kutumia viwanja vyetu, Kilimanjaro, Zanzibar, Dar es Salaam na Mbeya:-Mbowe
Kuhusu sera na mfumo mpya wa elimu uliozinduliwa juzi na Rais Jakaya Kikwete, Mbowe alisema tatizo la sekta ya elimu siyo sera, bali bajeti finyu na usimamizi mbovu.
MWANANCHI
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe ameiomba Serikali ya China kusaidia kuimarisha ufanisi wa mamlaka ya Reli ya Tanzania TAZARA.
Membe alisema anafanya mpango wa kukutana na Rais wa Zambia na kuandaa mapendekezo watakayoyawasilisha kwa Serikali ya China.
Alisema reli ya Tazara ni eneo linalotumika kwa kiasi kikubwa kuunganisha Mataifa hayo kiuchumi kwani Zambia haina bandari na hutumia reli hiyo kusafirisha bidhaa kutoka Dar es salaam kwenda Zambia.
Akizungumzia ukaribu wa Tanzania na China Membe alisema nchi hizi ni marafiki katika Nyanja mbalimbali na anaamini kuwa uhusiano huo utadumishwa kwa maendeleo ya Mataifa yote mawili.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameitaka Serikali kuacha siasa kwenye masuala ya kiuchumi, ukiwamo mgogoro kati ya Tanzania na Kenya kuhusu sekta ta utalii.
Akifungua kikao cha Baraza la Uongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Arusha jana, Mbowe aliwataka viongozi Serikali kutumia busara kushughulikia mgogoro huo ulioibuka baada ya Kenya kuzuia magari yenye usajili wa Tanzania kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
“Asilimia 40 ya watalii zaidi ya milioni moja wanaokuja Tanzania kila mwaka, hupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta,”
“Hatustahili kugombana nao, bali tunapaswa kutafuta namna bora ya kushirikiana. Tuna uwezo wa kuchagua marafiki, lakini kamwe hatuwezi kuchagua majirani. Hawa (Kenya) ni wenzetu, tutaendelea kuwa nao pamoja maisha yote.
“Tutunge sera nzuri ya usafiri wa anga na kuvutia kampuni kubwa za ndege kuja kuwekeza nchini kwa kutumia viwanja vyetu, Kilimanjaro, Zanzibar, Dar es Salaam na Mbeya,:-Mbowe.
Kuhusu sera na mfumo mpya wa elimu uliozinduliwa juzi na Rais Jakaya Kikwete, Mbowe alisema tatizo la sekta ya elimu siyo sera, bali bajeti finyu na usimamizi mbovu.
NIPASHE
Chama cha Wananchi (CUF), kimepuliza kipenga kwa wanachama wake kikiwataka wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi katika nafasi za udiwani, ubunge, uwakilishi na urais unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kadhalika, chama hicho kimeweka hadharani ratiba ya uchukuaji fomu, kura ya maoni, vikao vya kuchuja majina ya wagombea wenye sifa na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa ajili ya kufanya uteuzi wa wagombea uwakilishi, ubunge na urais.
Hata hivyo, ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu kwa nafasi ya urais kiporo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, jana jijini Dar es Salaam jana, Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Shewaji Mketo, alisema nafasi hizo zipo wazi kwa wanachama wote wenye sifa wanaotimiza masharti ya Katiba ya nchi na chama kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania.
“Chama kinatangaza kuwa kutakuwa na zoezi la kura za maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea wa udiwani, ubunge, uwakilishi na urais…uchaguzi huu utafanyika ili kukidhi matakwa ya Katiba ya chama Ibara ya 91,92 na 93 pamoja na marekebisho yake”:-Mketo.
Mketo alisema pamoja na chama hicho kuweka ratiba, malengo yao kama Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) yapo pale pale na kwamba kila chama kitatafuta wagombea katika ngazi zote na baadaye kuchambuliwa na vyama vya Ukawa ili kuona nani anastahili kupewa wapi ya kuwa mwakilishi wa Ukawa.
Vyama vinavyounda Ukawa ni CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na NLD.
HABARILEO
Kutokana na wahalifu waliopambana juzi na polisi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kutokamatwa, hali ya wasiwasi imeendelea miongoni mwa wakazi wa mjini hapa.
Sasa wananchi hao wameiomba Polisi kutoa tamko, kuhusu kikundi kilichorushiana risasi na askari Polisi na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja.
Aidha, wananchi hao wameitaka Polisi kutoa ufafanuzi kuhusu mwendelezo wa matukio mengi ya uhalifu wa kutumia silaha, ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi, ikiwemo kutokamatwa kwa watuhumiwa wa matukio hayo.
Hata hivyo, Msemaji wa Polisi, Advera, alisema Jeshi lake halina taarifa zaidi ya iliyotolewa juzi na Mkuu wa Opersheni wa jeshi hilo, Kamishna Paul Chagonja.
Habari za kipolisi zinasema kwamba bado wanaendelea kusaka wahalifu hao huku baadhi ya vikosi vya ulinzi na usalama, vimeongezwa kwa ajili ya kupambana na wahalifu hao. Juzi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi walipambana na kundi la wahalifu katika maeneo ya mapango ya Amboni na kusababisha wanajeshi wanne na polisi wawili kujeruhiwa.
Hata hivyo, kuna habari kuwa majeruhi mmoja ambaye ni mwanajeshi alifariki baadaye akiwa hospitalini. Habari zingine zinasema kwamba majeruhi wengine ambao ni polisi wanne na mwanajeshi mmoja, wanaendelea vizuri. Kuhusu mwanajeshi aliyekufa, polisi wamegoma kuzungumzia suala hilo, lakini habar
MTANZANIA
Wakati vita ya kuwania nafasi ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete ikipamba moto, baadhi ya wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanda ya Ziwa, wamemtaka Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, agombee urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Wananchi hao katika kutimiza dhamira yao, wamemtuma Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa, Dk. Raphael Chegeni, kwenda kumshawishi Lowassa ili awanie nafasi hiyo.
Mjumbe huyo wa NEC ya CCM, Wilaya ya Busega, alisema Lowassa anafaa kuwa rais hivyo atakwenda kumshawishi na atamchangia fedha za kuchukulia fomu ya kugombea kwa kushirikiana na marafiki zake ndani na nje ya CCM.
“Kati ya waliojitangaza kutaka wapitishwe na CCM kumrithi Kikwete, bado hatujaona mwenye sifa zinazotakiwa, sasa Dk. Chegeni kwa ushawishi wake tunamtuma akamwambie Lowassa akubaliane na matakwa yetu, achukue fomu ya kuwania urais kwani ndiye suluhisho la kero na changamoto za maisha ya Watanzania,” alisema mmoja wa makada hao kutoka mkoani Kagera kwa niaba ya wenzake.
Alisema kwamba, Lowassa amekuwa kimya muda wote licha ya kutajwa kwenye kinyang’anyiro hicho, lakini atamshawishi agombee nafasi hiyo kwa kuwa anaamini ana uwezo wa kuwatumikia Watanzania kutokana na rekodi yake ya utumishi wa umma alipokuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya nne.
DIRA YA MTANZANIA
Wakati Serikali ikihaha kutafuta mwarobaini wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika Mikoa ya kanda ya Ziwa,katika hali isiyokuwa ya kawaida imebainika watoto ambao huzaliwa wakiwa wamekufa huuzwa kwa waganga wa kienyeji.
Imedaiwa kuwa watoto hao huwa hawazikwi kama livo kawaida na taratibu za hospitali,badala yake wauguzi wa hospitali huwapeleka kwa waganga.
Tuhuma hizo zilitokea mbele ya Katibu tawala, Mwamvua Jilumbi katika kikao na wadau wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kukomesha vifo vya wajawazito na watoto Mkoani humo.
Wadau hao walieza kuwa viungo hivyo vimekuwa vikiuzwa kati ya 500,000 kiasi ambacho walieleza hutolewa na waganga hao.
JAMBOLEO
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mohamed Mpinga amesisitiza kuwa ni marufuku magari binafsi kuweka tinted kwenye vioo vya mbele kwa kuwa inakua vigumu kwa askari wa usalama barabarani kutambua aliyeko ndani ya gari.
Alisema kuwa madereva wengine wanakata sehemu ndogo kwa ajili ya kuangalia kioo cha pembeni na kama wanaweza kukata sehemu hiyo kwa nini washindwe kuacha sehemu ya mbele ili kuona vizuri.
“Gari inapikuwa na tinted inakuwa ngumu kutambua kwa urahisi nani yupo,na madhara yake hata kukiwa na majambazi huwezi kujua kwa urahisi..ni marufuku vioo vya mbele kuwa na tinted“:-Kamanda Mpinga
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook