MWANANCHI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kitaendesha operesheni mpya nchi nzima ikilenga kuhamasisha wananchi kudai kurejeshwa fedha zote ambazo zimeporwa katika kashfa mbalimbali za ufisadi badala ya kuachia wahusika kujiuzulu nafasi zao na wengine kufichwa.
Pia imesema operesheni hiyo maalum italenga kuamsha umma kutovumilia kashfa mbalimbali za wizi wa rasilimali za watu zinazoibuka kila mara,lakini hatua stahiki hazichukuliwi.
Naibu Katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu aliwataka wanan chi wa mjini na vijijini kujiandaa kwa operesheni hiyo iliyosisitiza kuwa itasaidia kuwaondoa Watanzania katika minyororo ya ufisadi unaozidi kuwafanya wawe maskini.
Alisema haitoshi kwa viongozi kukiri kuhusika au kulazimishwa kukubali au kutolewa kafara ili kuiokoa Serikali ya CCM kila kunapotokea kashfa kubwa ya wizi wa fedha zinazowanufaisha watu wachache na kuacha wengine wakifa kwa njaa bali nguvu ya umma inapaswa kutumika kuwaambia watawala kuwa imetosha.
Kongozi huyo alisema CCM inajua fedha hizo zilizoibwa Serikalini zinakwenda wapi na kudai kuwa mojawapo ya kutafuta fedha za kufanya kampeni ni kupitia kashfa za ufisadi.
MWANANCHI
Siku moja kabla ya kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali kuwasilisha bungeni ripotiya uchunguzi wa sakata la IPTL kuhusu ufisadi wa akaunti ya Escrow,Mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe amesema amekua akipata vitisho ili kuzuia ripoti hiyo.
Zitto alisema pamoja na vitisho hivyo haogopi kwa kuwa maisha yake ameshayaweka nadhiri siku nyingi.
“Kuna kundi la wahuni kutoka Musoma limeletwa hapa Dodoma likiongozwa na mtu mwenye rekodi ya ujambazi,hivi sasa anashikiliwa na Polisi kwa kukutwa na nyaraka zilizoibwa ofisi ya bunge,usalama wa wajumbe wote wa PAC upo shakani,”alisema Zitto.
Aliongeza kuwa kuna vipeperushi vimesambazwa kumkashifu lakini havimsumbua kwa kuwa yeye anataka ukweli ujulikane.
Baadhi ya Wabunge jana walikua na vitabu vilivyoandikwa ‘Mjue Zitto Kabwe kama mtetezi wa wanyonge’ lakini ndani yake kuliandikwa maneno ya kumkashifu Mbunge huyo.
MWANANCHI
Polisi kanda ya Dar es salaam wametoa tahadhari kwa wanawake kuacha kushiriki mapenzi na watu wasiowafahamu ili kuepuka kuuawa.
Taarifa ya Kamishna wa Kanda Suleiman Kova ilisema wasichana hususani wa jijini Dae es salaam wanatakiwa kuwa makini na wanaume wasiowajua kwa sababu wengi wameishia kuuawa kikatili huku miili yao ikitelekezwa hovyo.
“Kuna taarifa ya kuwepo wanaume wawili wanaowashawishi wanawake kufanya nao mapenzi na baada ya muda huwaua,natoa tahadhari kwa wanawake wote kuwa makini na watu hawa”alisema Kova.
Alisema siku za hivi karibuni kumekuwepo na matukio mengi ya mauaji ya aina hiyo ambapo kwa sasa wanawake wapatao sita tayari wameshapoteza maisha.
MWANANCHI
Mtoto mlemavu wa akili na miguu mwenye miaka14 anadaiwa kubakwa na kuambukizwa magonjwa ya zinaa na mwanaume mwenye umri wa miaka50.
Mwanaume huyo anadaiwa kufanya kitendo hicho siku moja kabla ya kufunga ndoa na mke mpya aliyemlipia mahari eneo la Uyole Mbeya baada ya kuachana na mke wake wa kwanza aliyezaa naye watoto zaidi ya watatu.
Tukio hilo lilitokea November 4 na kuripotiwa kituo cha polisi ambapo mpaka sasa mtuhumiwa anasakwa na polisi kwa ajili ya ufunguliwa kesi ya kubaka.
Shangazi wa mtoto huyo akizungumza kwa masikitiko alisema waligundua mtoto wao amefanyiwa kitendo hicho baada ya kutoka kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo huku akilia na walipomchunguza ndipo walipobaini kuwa amebakwa na vipimo vilionyesha ameambukizwa magonjwa ya zinaa.
NIPASHE
Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo ametajwa kuwa na uhusiano wa karibu na mmoja kati ya vijana wawili waliokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa tuhuma za kuiba nyaraka za ripoti ya ukaguzi wa hesabuu zaidi ya bilioni300 zilizochotwa kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyoko benki kuu ya Tanzania BoT.
Wakazti Waziri Muhongo akitajwa kuwa na uhusiano wa karibu na mtuhumiwa huyo,Spika wa Bunge Anne Makinda jana ilikua ni siku yake ya kwanza kuongoza bunge tangu lianze November4,anadaiwa kutajwa kuwa kwenye orodha ya vigogo waliovuna fedha hizo huku yeye akipata mgawo wa dola za Marekani milioni moja.
Aliyemtaja Waziri Muhongo kuwa na uhusiano wa karibu na kijana huyo ni Bunge wa Ubungo John Mnyika wakati akichangia mjadala kuhusu muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka2014.
Madai hayo ya Mnyika yalitolewa siku moja baada ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Msiime kusema kuwa katika mahojiano na kijana huyo alikiri kuwa amepewa na Mbunge mmoja ambaye hakumtaja jina ili kuepusha kuharibu upepelezi unaoendelea.
NIPASHE
Waziri wa ujenzi Dk. John Magufuli mradi wa mabasi yaendayo kasi DART awamu ya kwanza katika barabara ya Morogoro unatarajiwa kuanza Machi,mwakani.
Magufuli alisema mradi huo kwa sasa upo katika hatua za mwisho na ifikapo Machi mwakani utakua umekamilika na utaanza kutumika rasmi.
Alisema upanuzi wa barabara hiyo utaanza Dar es salaamna utakua na umbali wa kilomita200 na Wizara imetenga kiasi cha milioni100 kwa ajili ya maandalizi.
Alisema mradi huo ambao utatumia dola za Marekani milioni290 uliofadhiliwa na benki ya dunia utekelezaji wa pili umegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni chalinze na Tanga
HABARILEO
Katika hali isiyoua ya kawaida wanaume watatu,wawili wakazi wa jijini Mwanza walizua tafrani baada ya kung’ang’nia maiti ya Happy Wangoge Mathias mwenye umri wa miaka 33 aliyekufa siku chache baada ya kufunga ndoa na Pascal Mayalla.
Hiyo inatajwa ilikua ndoa ya tatu ya marehemu huyo anayedaiwa alikua ni mke wa mtu na kwamba aliolewa na mahari ya ng’ombe 11 na mwanaume Chanjo Ryoba mkazi wa Nyamongo Wilayani Tarime aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 14.
Tukio la kuing’angania maiti hiyo lilianza rasmi jumamosi iliyopita baada ya mke huyo kufariki dunia ambapo inasemekana enzi za uhai wake,Happy alikua akiishia Jijini Mwanza na ujihusisha na biashara ya samaki na aliolewa tena na Benjamini Bushoti kabla ya hivi karibuni kufunga ndoa ya kikristo na Mayalla.
Aliyeanzisha vurugu hizo ni mumewe wa pili ambaye alikua akiishi naye na alizaa naye watoto wawili kabla ya kufunga ndoa na Mayalla ambapo uvumilivu ulimshinda baada ya kuwaeleza waombolezaji yeye ndiye mume halali wa marehemu na alikua akiishi naye pamoja na watoto wao wawili.
Kufuatia tukio hilo watu mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa mtaa walimtuliza mume huyo wakimsihi aache vurugu ili waangalie hoja iliyokua mbele ya kuandaa safari ya mwisho ya kwenda kumzika marehemu.
HABARILEO
Seikali imesema itatoa tena usajili wa namba zote za simu za mkononi ili kuthibitisha zinazotumikana ambazo ni feki ilikuwabaini wezi wanaotumia majina si yao.
Naibu Waziri wa Mawasiliano January Makamba alikiri kuwa wapo wanatumia majina feki kwa kusajili namba zao za simu za mkononi jambo ambalo ni kinyume na sheria.
“Wapo watu wanaotumia majina na vitambulisho feki wanaposajili namba zao,tunaomba tuungwe mkono tutakapotangaza usajili mpya wa namba za simu kwani itakua na faida kwa wananchi wote,”alisema Makamba.
MTANZANIA
Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono amekiri kulishwa sumu alipokua jijini London Uingereza,huku akihusisha tukio ilo na wabaya wake dhidi ya sakata la kampuni ya kufua umeme IPTL inayotuhumiwa kuchota zaidi ya bilioni300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
“Tulikua watu tusiopungua11 katika kazi hii kama kamati,tuliondokea Dar es salaam tukakatiwa tiketi na Serikali,kitu ambacho kilishtusha wengi ni jinsi nilivyougua gafla kabla ya kutoka uwanja wa ndege wa JNIA,nilipata ujumbe wa simu lakini siwezi kusema ulitoka wapi”alisema Mkono.
Alisema wakiwa nchini Uingereza alifikia hotel ya Crown Plaza ambapo hufikia kila wakati huku wabunge wenzake wakifikia Park Hotel na walitakiwa kutembelea bunge la nchi hiyo ambapo yeye aliomba kwanza kwenda ubalozi wa Tanzania na badaye akakutana na wenzake huko bungeni.
“Tukaanza kuulizwa maswali,baadaye gafla hali yangu ikabadilika,nikapoteza fahamu kabisa,hayo nimeambiwa sikuwa naelewa kabisa,nikamwambia kiongozi wa msafara Willium Ngeleja hali yangu ni mbaya wanirudishe nyumbani lakini badala yake wakanipeleka hospitali.
Alisema baada ya daktari wake kumchungaza akasema itakua ni sumu na hata baada ya kupimwa ilionekana damu yake ina sumu nyingi na ililenga kuharibu figo yake.
Alisema kabla ya kuondoka Dar alipata chai na wabunge wenzake kwenye hotel iliyopo uwanja wa ndege hata hivyo hawezi kujua i wakati gani na mahali gani sumu iyo liwekwa.
MTANZANIA
Zaidi ya wanafunzi100 wa Shule ya Msingi Hananasif na Mkunguni za Wilayani Kinondoni,Dar es salaam wanadaiwa kulawitiwa na wanaume kwa nyakati tofauti.
Taarifa zilieleza kuwa wanafunzi hao wa darasa la kwanza hadi la nne wanaosoma madarasa tofauti wanafanyiwa vitendo hivyo nje ya shule na maeneo wanayotoka.
Kutokana na taarifa baadhi ya wazazi na hata taasis za Serikali na uongozi wa shule ya Hananasifulilazimika kuitisha vikao vya dharura kujadili suala hilo.
Chanzo cha kuaminika kutoka ,shuleni hapo kilidai mwalimu mkuu hiyo aliwaita wanafunzi kadhaa na kuwahoji na baadhi yao walikiri na kuw ataja wnaaume wanaowafanyia vitendo hivyo na mahali wanapofanyia.
Baadhi ya wanafunzi hao walisema aliwahi kufanyiwa kitendo hicho nyumbani kwao na alishahojiwa na mwalimu wake mkuu na kumweleza ukweli huku mwanafunzi mwingine wa kiume wa darasa la pili alidai huwa anafanyiwa na kijana mmoja ambaye humpa vitumbua.
“Mimi nilifanyiwa muda kidogo, nimesahau siku,wakati narudi nyumbani nilikutana na mtu kichochoroni akanifanyia hivyo lakini nilimwambia mama na akanimabia nikatoe taarifa kituo cha polisi
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook