MWANANCHI
Mwanzilishi wa kanisa la Pool of Siloam,Nabii Eliya Adam amefariki dunia juzi mchana muda mfupi baada ya kuwaeleza wasaidizi wake siku hiyo ndiyo ilikua ya mwisho kwake kuishi duniani.
Nabii huyo alianzisha kanisa hilo mwaka 2003 katika eneo la Mbezi Beach Dar es salaam na baadaye kuenea maeneo mbalimbali nchini kote.
Akitoa taarifa ya kifo cha Nabii Eliya,kuhani kiongozi wa kanisa hilo alisema kabla ya kifo cha nabii huyo aliwaita na kuwaambia mambo manne ikiwemo kuhakikisha wanajenga makanisa ya kutosha na kuwataka waumini wa kanisa hilo kukamilisha kila jambo walilopanga.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Jakaya Kikwete kulivunja baraza la Mawaziri na kuunda jipya kutokana na tuhuma mbalimbali za ufisadi.
Alisema ni lazima hatua hiyo kuchukuliwa ili kukabiliana na ufisadi vinginevyo kambi ya upinzani bungeni itawasilisha hoja ya kutokua na imani naye.
Alisema Serikali imekua ikishindwa kuchukua hatua za ufisadi ambazo zinawakabili watendaji wake na kusisitiza ni bora Rais amfukuze kazi Waziri mkuu Mizengo Pinda na Maziri wake kutokana na kutowajibika kwao.
NIPASHE
Muhitimu bora wa chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 2014 Doreen Kabuche mwenye miaka22 aliushangaza umma uliohudhuria mahafali ya44 ya chuo hicho baada ya kutangazwa kuwa kinara kwa ufaulu baada ya kupata alama A 32 na B+ sita kati ya masomo 38 ya shahada ya takwimu bima (Actuarial Science),
Kwa alama hizo Doreen alipata wastani wa alama za ufaulu GPA 4.8 na kuacha alama ya 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu cha alama tano hivyo kupata shahada ya kwanza daraja la kwanza.
Doreen alisema alihitimu shahada hiyo akiwa miongoni mwa wanafunzi28 wa darasa lake lakini akihitimu sambamba na wanafunzi wengine zaidi ya elfu tano wanawake wakiwa ni 2,298 wa shahada ya kwanza.
Tofauti na fikra za wengi ambao huamini mwanafunzi bora hutoka katika shule zinazotoza ada kubwa na kutumia kiingereza kama lugha ya mawasialino kwani Dorfeen alipitia katika shule za kawaida kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita,
NIPASHE
Saratani ya mapafu na kinywa zimetajwa kuongoza kwa kushambulia wanaume umetafiti umeonyesha huku ukibainisha kuwa wanawake hushambuliwa na saratani ya kizazi pamoja na maziwa.
Mtalaam wa saratani Sanjay Maitra anasema ukosefu wa vifaa na uelewa mdogo wa watu nchini Tanzania ndio vimechangia ugonjwa wa saratani kuwa hatari zaidi.
“Ni jukumu la kila mmoja katika jamii kupambana na magonjwa kama haya yanayozonga familia zetu kwani katika miaka10 iliyopita njia za matibabu ya ugonjwa wa kansa ijulikanayo kama Multiple Myeloma zimeongezeka na kuleta matumaini kwa wagonjwa wa aina hiyo ya kansa.
Alisema kumekua na ongezeko kubwa la wanaume kuugua saratani ya mapafu inayotokana na uvutaji wa dawa za kulevya huku wana wake nao wakisumbuliwa na kansa ya kiuzazi ambayo nayo inakua kwa kasi.
JAMBOLEO
Wavuvi haramu waliokua wakijaribu kuvua katika kisiwa cha Karange ,Tanga kwa kutumia baruti wamejeruhiwa na kukatika viungo vya miili yao.
Tukio hilo lilitokea November 12 baada ya kulipuliwa na kujeruhiwa na baruti hiyo na kuumia sehemu mbalimbali huku wakiwa katika hali mbaya.
Chombo kilichokua kikitumika kwenye uvuvi huo haramu ni Ngalawa na majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Bombo ambapo hali zao zimeelezwa kuwa ni mbaya sana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Frasser Kashai alithibitisha kupatikana kwa majeruhi hao na kusema upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao wa wahalifu hao wa uvuvi haramu.
JAMBOLEO
Serikali imesema mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro iko mbioni kufa na kuleta aibu kwa Taifa baada ya kupoteza hadhi yake ya kuwa urithi wa Dunia iliyopewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu ya Sayansi na Utamaduni UNESCO kutokana na ongezeko kubwa la watu na mifugo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alisema ongezeko la watu katika hifadhi ya Ngorongoro ni kubwa na imekua tishio kwa hifadhi hiyo kuendelea kuwepo kwa siku zijazo.
Nyalandu alisema idadi ya magari na watalii wanaotembelea mamlaka hiyo ni kubwa na imekua ikitosheleza hitaji la hifadhi hiyo lakini idadi kubwa ya makazi ndani yake na mifugo ni tatizo ambalo linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi haraka sana kwa kuwa wamekua wakiharibu mazingira.
Alisema Serikali imeandaa mpango wa kuinusuru hifadhi hiyo pamoja na mpango wa kuhama kwa hiari na kwamba hivi sasa ipo kwenye mazungumzo na wadau mbalimbali wa utalii ili kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kuendeshea kazi hiyo.
MTANZANIA
Utafiti umeonyesha kuwa kipimo binafsi cha Virusi vya Ukimwi kinachotumiwa na watu wengi majumbani hakitoi majibu sahihi.
Mwakilishi wa Shirika la kimataifa la Utafiti wa Afya Afrika AMREF uliotolewa mwaka jana umebaini kipimo hicho ambacho kinauzwa kati ya 5,000 na 6,000 matokeo yake si ya kweli kwa asilimia 100.
Alisema majibu hayo hupatikana kati ya dakika20 hadi40 na watu wengi wanapenda kukitumia kwa sababu kinawapa nafasi ya kukitumia wakiwa nyumbani na pia kina usiri kwa kuwa watu wengi hawataweza kujua matokeo yao.
Alisema kipimo hicho hupima chembe zinazozaliwa baada ya virusi kuingia mwilini amba zo ni matokeo ya mwili kuzalisha vizuia virusi na si virusi vyenyewe.
MTANZANIA
Waziri mkuu,Mizengo Pinda leo anatarajia kuwasilisha kwa spika wa Bunge Anne Makinda ripoti ya uchunguzi kuhusu kashfa ya uchotwaji wa shilingi milioni200 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokua imefunguliwa na benki kuu ya Tanzania BoT.
Mbali na hilo,pia leo jioni atakutana na kamati ya uongozi wa Bunge na kueleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali katika kukomesha mauaji ya wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto,Mkoani Manyara tangu yalipozuka hadi sasa.
Katika kikao hicho pia itapokea maelezo ya waziri mkuu kutokana na madai ya Wabunge kuwa uwajibikaji wa Serikali umekua ukidorora wakati ikielekea ukingoni mwa uhai wake.
Mwenyekiti wa Bunge Azzan Zungu alitangaza uamuzi huo jana baada ya kamati hiyo kumaliza kikao cha kujadili hoja hizo zilizowasilishwa bungeni.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook