Ni kawaida kwenye Mabunge mbalimbali duniani kuona Wabunge wametolewa nje au wenyewe wametoka nje lakini ni nadra sana kusikia Waziri mkuu kazingua bungeni na kusababisha Spika kuamuru atoke nje.
Imetoka huko New Zealand ambapo waziri mkuu mpya John Key ametolewa bungeni baada ya kukaidi kufata kanuni za bunge hilo ambalo limekua na mjadala mkali kuhusu ishu ya akaunti za siri ambazo zinadaiwa kuwepo kwenye kisiwa cha Panama.
Spika wa Bunge David Carter ametetea maamuzi yake na kusema waziri mkuu alikaidi onyo la kuheshimu kanuni za bunge na hivyo hakua na kinga ila kumuadhibu kama anavyofanya kwa Wabunge wengine.
BBC wameripoti kwamba rekodi za bunge zinaonyesha Waziri Mkuu huyu aliwahi kutolewa bungeni mara tatu wakati akiwa mbunge lakini pia hii sio mara ya kwanza kwa Waziri mkuu wa NewZealand kutolewa bungeni, Waziri mkuu wa zamani Helen Clark alitolewa mwaka 2005 vilevile David Lange kwenye miaka ya 1986 na 1987.
ULIKOSA KUONA YA WABUNGE WANAWAKE UKAWA WALIVYOTOKA NJE YA BUNGE WAKIKATAA KUITWA ‘BABY’ ? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI