Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.
#NIPASHE Moto wawaka kashfa ya kontena 100 zilizodaiwa kuvushwa bila kukaguliwa bandarini, wafanyabiashara 10 wajitokeza kutoa maelezo pic.twitter.com/PWJmN4htUN
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#NIPASHE Serikali imetishia kuachana na washirika wa maendeleo wanaotoa misaada yenye masharti yasiyotekelezeka na yanayotishia usalama nchi pic.twitter.com/bIbNGcXmKB
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#NIPASHE BoT imesema matumizi ya fedha za kigeni km dola, pauni na Euro, hayasababishi kushuka au kuifanya shilingi ya kitanzania kutetereka pic.twitter.com/DBj6DDhUHo
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#MWANANCHI Imebainika watoto 50 wenye umri kati ya miaka minane na 12 waliopimwa, 20 wameingiliwa na kuambukizwa magonjwa ya zinaa Moshi pic.twitter.com/vy4ZHErwHT
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#MWANANCHI Tanzania yakataa visa moja EAC, sababu ni kutoridhishwa na masuala mbalimbali ikiwamo la usalama hasa tishio la ugaidi pic.twitter.com/p0cwB2fx8C
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#MWANANCHI TPDC yakamilisha mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam pic.twitter.com/DJqVWN26EU
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#MTANZANIA Samaki mkubwa aonekana Kilwa, ana urefu wa futi 25, ngozi ngumu mithili ya tembo, hakatiki kirahisi kwa shoka wala panga pic.twitter.com/g3YULYVWvr
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#MTANZANIA Wamachinga, polisi Mwanza wapambana nje ya msikiti ni baada kutaka kuwaondoa eneo hilo kutokana na kukwamisha shughuli za ibada pic.twitter.com/8Ja8gpUKIV
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#NIPASHE CAF imetoa viwango vya ubora wa klabu Afrika, huku Yanga ikiongoza kwa klabu za TZ, Yanga ni ya 331, Azam FC- 351 na Simba-356 pic.twitter.com/Xc24WHM5fV
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#MWANANCHI Uondoaji wa magugu maji ktk ziwa victoria ni miongoni mwa miradi minne iliyotafuna zaidi ya bil 8 pic.twitter.com/dnTwvp1AdV
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#MAJIRA Rais Shein aagiza wakuu wa mikoa sita waliofanya vibaya ktk utekelezaji wa fedha za kukopesha vijana wachukuliwe hatua kali pic.twitter.com/V9hT3bYzOM
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#JamboLEO Daktari wa mifupa MOI, Dk Bryceson Mcharo asema wasichana hatarini kupata kibiongo kuliko wavulana, asema zipo homoni zinachangia pic.twitter.com/aZ3sWFjcB3
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#HabariLEO Kwa mara nyingine tena mahakama ya rufaa Tabora imetupa maombi ya Kafulila ya kupinga matokeo ya Ubunge jimbo la Kigoma Kusini pic.twitter.com/cmarD0lFvQ
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#MWANANCHI Wakati Kampuni ya Samsung ikitahadharisha wateja wake kuhusu simu za Samsung Galaxy Note 7, imebainika zinauzwa kariakoo, Mwenge pic.twitter.com/HsQCbb4sXq
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#MWANANCHI TPA yajitoa ktk mradi wa upanuzi wa bandari ya Mtwara, yasema hairidhishwi na tathmini ya thamani ya ardhi na kiwango cha fidia pic.twitter.com/zkZAKGQX70
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
#NIPASHE EWURA imepiga marufuku watu binafsi kumiliki vituo vya mafuta kwenye yadi zao na kwamba sheria hairuhusu jambo hilo pic.twitter.com/Vkyxom7v2C
— millardayo (@millardayo) October 15, 2016
YALIKUPITA MAGAZETI OCTOBER 15 2016? MOTO KUWAKA KASHFA YA KONTENA 100 BANDARI, BoT KUTETEA MATUMIZI YA DOLA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI