Moja ya vilio vikubwa sehemu za kazi ni pale ambapo inatokea teknolojia halafu inachukua nafasi ya kazi za watu kama utani!
Zilipokuja computer ilikuwa zengwe, wapo ambao walijikuta hawana ajira sasa hii kutoka Ujerumani imenishtua kidogo.
Kampuni ya kutengeneza magari Ujerumani ya Daimler imejipanga kutengeneza gari ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kujiendesha yenyewe huku ikiwa na uwezo wa kuchukua abiria wanne.
Gari hii ambayo imeundwa kwa muundo wa kisasa itakuwa ya kipekee huku ikiwa na usukani kama magari mengine tofauti na lile gari la google ambalo halina usukani, hili lina siti ya dereva na siti za abiria, siti zote zina uwezo wa kugeukiana na kufanya watu waliokaa ndani ya gari kutazamana kama wako kwenye meza moja.
Gari hii aina ya Mercedez-Benz Luxury Sedan F 015 bado haijapangiwa tarehe ya kutengenezwa na kuzinduliwa lakini Mkurugenzi wa Daimler ambaye alikuwa anaelezea gari hilo huko Las Vegas kizazi kijacho cha magari kitakuwa na magari ambayo yana uwezo wa kumpa kila mtu fursa ya kustarehe wawapo ndani ya gari.
Usipate shida, video hii hapa cheki mwenyewe itakavyokuwa.
https://www.youtube.com/watch?v=DYTV4d-Gn0s