Mchezaji aliyekuwa tegemezi kwenye mechi za kombe la dunia za timu ya Brazil Neymar Jr, hatimaye amepelekwa kwao Guaruya, Sao Paulo kwa ajili ya mapumziko. Neymar amepata matibabu baada ya kupata maumivu kwa kugongwa kifuti kwenye uti wa mgongo na mchezaji wa Colombia wakiwa uwanjani.
Neymar alipelekwa na helicopter kwenye uwanja wa mazoezi ambapo alikutana na wachezaji wenzake, baadae alikutana na waandishi pamoja na mashabiki na safari ikaelekea Sao Paulo.