Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameviagiza vyombo vya usalama nchini kufanya uchunguzi na kuwakamata mara moja watu wanaoichafua Serikali kwa kusambaza mitandaoni vitabu ambavyo sio sahihi.
“Nimepata nafasi ya kuona kitabu cha darasa la tatu kilichokuwa na makosa ambayo yamekwishafanyiwa marekebisho na wahusika wamechukuliwa hatua lakini pia kipo kitabu kinachosambaa kikionesha mwili wa binadamu na mishale imewekwa hovyo hovyo kitabu hicho hakijawahi kuwa sehemu ya vitabu vilivyotolewa na Serikali”-Waziri Ndalichako
“Nasikitika sana kuona watu wameamua kutunga vitu ambavyo vinalengo la kuichafua Serikali wakijua ni kosa la jinai, naviagiza vyombo vya usalama mara moja vitafute watua ambao wanaichafua Serikali ili wachukuliwe hatua” –Waziri Ndalichako
MAZISHI YA MDOGO WAKE HECHE: “HATUTAKI FIDIA” – HECHE