Rubani na abiria mmoja inasadikika wamefairiki Dunia, katika ajali ndege ya Kampuni ya Auric Air, kufuatia kuanguka asubuhi ya leo katika Uwanja wa ndege mdogo Seronera, Serengeti.
Ndege ndogo ya Shirika la Auric Air imepata ajali katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.
Ajali hiyo imetokea saa 1:30 asubuhi ambapo ilikuwa ikiruka kutoka Serengeti kwenda Arusha baada ya kushusha watalii.
Katika ajali hiyo, rubani na abiria mmoja wamefariki dunia, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete akizungumza na AyoTV na millardayo.com amethibitisha kutokea ajali hiyo.
“Tunatoa taarifa zaidi baadaye kwani sasa kazi inayoendelea ni kuokoa vitu na kuhifadhi miili,” Pascal Shelutete
KUTANA NA ‘UKUTA WA HESHIMA’ WA SUGU ALIOUTENGENEZA HOTELINI KWAKE