Mwili wa Mwanajeshi mmoja, vijana 10 wa JKT na Wafanyakazi wawili wa basi la Igunga Express waliofariki June 14 mwaka huu katika eneo la maili tano mtaa wa Igodima Mbeya itaagwa kesho katika kambi ya JKT Itende
Akizungumza na waandishi wa Habari leo June 18, 2018 katika ukumbi wa JKT Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Jeshi la Wananchi (JWTZ ) Kanali Ramadhan Dogoli amesema taratibu zote zimekamilika.
Nimekuwekea PICHA na MAJINA ya vijana waliofariki katika ajali hiyo.
Miili ya Wanajeshi 11 na wengine 3 waliofariki ajalini kuagwa kesho Mbeya