Wimbi la matukio ya kinyama dhidi ya walemavu wa ngozi yameendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali hapa nchini hususani Mikoa ya Kanda ya Ziwa na kila kukicha bado taarifa zimeendelea kutolewa huku bado ufumbuzi ukionekana kutofikiwa muafaka.
Pamoja na adhabu ambazo hutolewa na vyombo vya dola dhidi ya wahusika lakini imeonekana kama sikio la kufa kwani bado tunaendelea kushuhudia matukio yanayofanana na hayo yakishamiri ndani ya jamii
Mmoja wa waliokua wakifanya biashara haramu ya ngozi za binadamu aliyenusurika adhabu ya kunyongwa mwaka 2002 ambaye hakutaka kutaja jina lake amekutana na Gazeti la MTANZANIA na kufichua siri za namna biashara hiyo inavyofanyika hapa nchini kwa usiri mkubwa huku kukiwa na mtandao mkubwa ndani yake.
Sambamba na hilo pia ameelezea jinsi wanamtandao wa biashara ya ngozi walivyosambaa katika nchi jirani ambao hushiriikiana katika biashara hiyo.
Akitokea Mkoa wa Mbeya alisema alianza biashara hiyo toka mwaka 1997 baada ya kuacha biashara ya baa ambapo alikutana na wafanyabiashara wa ngozi za binadamu toka sehemu mbalimbali.
Alisema wateja wao wakubwa walikua ni matajiri wanaomiliki migodi ambao maskani yao ni porini pamoja na majamba ambao hata hivyo hajui walikua wakizipeleka wapi na kufanyia shughuli gani kwa wakati huo.
Alisema biashara hiyo ni ngumu sana kwani unatakiwa kuwa jasiri sana na hufanyika kwa usiri mkubwa ambapo huua watu na kisaha kuwachuna ngozi kabla ya kwenda kuziuza kwa bei nzuri ambayo hakua tayari kuiweka hadharani.
Alisema aliponea kunyongwa na mpaka sasa hajui aliachiwaje huru huku akikaa gerezani kwa miaka minne na alikutana na mateso ya aina yake huku akizimia kwa siku mbili mfufulizo bila msaada wowote kutokana na kipigo na wenzake wanne wakaishia adhabu ya kunyongwa.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook