Ni habari mbili zinazoihusu ofisi moja lakini zimetoka kwenye Ofisi mbili tofauti, IKULU Dar es salaam kwa Rais Magufuli huku nyingine ikitoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Taarifa ikufikie kwamba Rais John Pombe Magufuli leo amemteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dr. Sophia Kongela kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC.
Wakati huohuo kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amemteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dr. Maulid Banyani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo la Nyumba NHC.