Ni kesi ambayo ipo Mahakamani Kisutu Dar es salaam kuhusu yule Mkazi wa Chato mkoani Geita aliyetuhumiwa kwa kuandika habari za uongo Facebook kuhusu kampuni ya Acacia na Serikali.
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imeipiga kalenda kesi hiyo inayomkabili Mkazi huyo wa Geita Obadia Kiko mwenye umri wa miaka 41 hadi November 14, 2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika.
Mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la kuchapisha taarifa ya uongo kupitia mfumo wa kompyuta na kuweka kwenye mtandao wa Facebook, kinyume na sheria ya makosa ya Mtandao Namba 14 ya mwaka 2015.
Inadaiwa kuwa August 3, 2017 akiwa maeneo ya Chato Geita aliandika kwenye Facebook taarifa ifuatayo >>> “Taarifa kutoka kikao cha mazungumzo kati ya Serikali na Wawakilishi wa Kampuni ya Acacia kuwa Wanasheria wetu wanashindwa kutafsiri vifungu vya sheria hadi kufikia kuomba msaada kwa Wanasheria wa Acacia, sasa hivi ni vituko mwizi anakusaida sheria hahahaaaa”
Mazungumzo bado yanaendelea lakini Wanasheria wetu wanabanwa sana ukizingatia wale jamaa wana vielelezo vyote vya mikataba, kiukweli tumuombe Mungu maana Serikali ikitaka kuvunja mkataba na Acácia gharama kubwa zitatuhusu.
Lakini pia kuendeleza uvyama utatugharimu sana baada ya Mh.Rais Magufuli angewashirikisha wakina Mawakili wasomi waliokuwa wakali Tundu Lissu, Kibatala na Fatuma Karume kwenye mambo muhimu kama haya yeye kaleta Uchama sasa itatugharimu.
ULIPITWA? Hii ni Tahadhari kwa Ma-admin wa group za WhatsApp Tanzania
ULIPITWA? Tazama hapa Hoteli aliyojenga Mbunge Mr. II Sugu Mbeya… bonyeza play kujionea
UNATAKA KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI? Breaking NEWS, Za Mastaa, Siasa, Michezo na nyingine…. fanya jambo moja tu rahisi… BONYEZA PAGE ZIFUATAZO ili nikutumie kila kitu kiganjani mwako >>> INSTAGRAM <<<< FACEBOOK >>>> TWITTER >>> pia bonyeza SUBSCRIBE HAPA >>> YOUTUBE