Jumanne ya March 27 2018 uwanja wa Taifa Dar es Salaam utachezwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Congo DRC, huo ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliyopo katika kalenda ya FIFA.
Kuelekea mchezo huo naomba ni kujulishe dondoo muhimu
1- Timu ya taifa ya Congo DRC imewasili Tanzania leo ikiwa na kikosi cha wachezaji 26, kati ya hao wanne tu ndio wanacheza Ligi za Afrika waliosalia ni nje ya bara la Afrika wakati Tanzania ni Mbwana Samatta pekee ndio anachezaji nje ya bara la Afrika katika kikosi cha Taifa Stars.
2- Tanzania ina wachezaji wanne pekee wanaocheza nje ya mipaka ya Tanzania waliyomo katika kikosi cha Taifa Stars kwa sasa ambao ni Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Simon Msuva wa Difaa El Jadid ya Marocco, Mandawa anayecheza Botswana na Samatta anacheza Genk ya Ubelgiji.
3-Tanzania wao wapo nafasi ya 146 katika viwango vya soka vya FIFA vinavyotolewa kila mwezi wakati Congo DRC wao wapo nafasi ya 37 katika viwango vya soka vya FIFA.
4- Congo DRC ndio timu ambayo ina mchezaji ghali zaidi katika bara la Afrika Cedric Bakambu ambaye ameweka rekodi ya mchezaji wa Afrika pekee aliyesajiliwa kwa dau la pound milioni 65 akitokea Villareal ya Hispania na kujiunga na Beijing Guoan.
5- Katika List ya wachezaji 26 wa Congo DRC waliyokuja kucheza na Taifa Stars Jumanne ya March 27, wachezaji 14 pekee kati ya 26 wa Congo ndio wamezaliwa Congo wengine wote wamezaliwa Europe.
EXCLUSIVE: Kingine usichokifahamu kutoka kwa Victor Wanyama wa Tottenham