Baada ya wiki kadhaa kupita toka taarifa zisambae katika mitandao ya kijamii kuwa aliyekuwa beki wa Yanga SC Hassan Kessy ameituhumu timu yake hiyo kutomjulisha hatma yake hadi dakika ya mwisho ya dirisha la usajili Tanzania likifungwa.
Hassan Kessy ambaye alikuwa anaituhumu Yanga kama ilikuwa na lengo la kutotaka apate timu mpya msimu 2018/19, leo August 3 2018 zimeripotiwa taarifa za beki huyo kusaini nchini Zambia.
Kessy leo ameripotiwa kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia club ya Nkana Red Devils ya Zambia, club ya Nkana kama huifahamu tu ilianzishwa mwaka 1935 ikiitwa Rhokana United FC kabla ya miaka ya 1990 kubadilishwa jina na kuitwa Nkana Red Devils ipo Kitwe Zambia.
PICHA: BoiplusMedia
“Nimeenda chumbani kwa Canavaro, alichonijibu SINTOSAHAU”-Edo Kumwembe