Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema, ni kosa kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na Kampuni ya QNET kisha kudai wametapeliwa.
Ameeleza hayo jana baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Geita kurejesha Tsh. Milioni 5.48 kwa Mwalimu Rose Mgomba aliyedai kutapeliwa.
Mganga amesema, urejeshwaji wa fedha hizo ni kosa kisheria kwa sababu biashara iliyokuwa inafanywa na kampuni hiyo ni Upatu Haramu.
“Ni kosa kisheria kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na Kampuni ya Qnet kisha kudai wametapeliwa kwakuwa kufanya hivyo ni kosa,” Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Biswalo Mganga