Serikali imeeleza kuichukulia hatua kampuni yoyote ya Mawasiliana ambayo itaruhusu mteja wake kusajili laini ya simu kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine na kusisitiza kuwa zoezi la kuzifunga laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa kutumia alama za vidole linaendelea.
Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akizundua mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Kibuye Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.
RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MAKUBWA RC MWANRI ASTAAFU, GONDWE, ANDENGENYE WAGUSWA NA WENGINE