Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameagiza Daktari aliyejimilikisha hospitali ya serikali kwa muda kujitajirisha binafsi achukuliwe hatua kali.
Waziri wa Afya ametoa agizo hilo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Dar es Salaam alipotembelea Hospital ya Amana kujionea utendaji kazi.