Kwa mujibu wa shirika la habari la sky news takriban mateka 240 waliotekwa nyara mnamo Oktoba 7 walitoka katika jamii zikiwemo mashamba ya pamoja na kambi za kijeshi kusini mwa Israel pamoja na watu waliohudhuria tamasha la muziki.
Zaidi ya nusu walikuwa na uraia wa kigeni na wa nchi mbili kutoka nchi 40 zikiwemo Uingereza, Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Uhispania, Ureno, Thailand, Argentina na Chile, kulingana na serikali ya Israel.
Hadi 40 kati yao ni watoto, akiwemo mtoto mchanga wa miezi 10, vyombo vya habari vya Israel vimesema, pamoja na wanajeshi, wazee na watu wenye ulemavu.
Serikali ya Israel imesema mateka wawili walipatikana wakiwa wamefariki katika mji wa Gaza.
Mrengo wa kijeshi wa Islamic Jihad, Brigedi za al Quds, ulitangaza kifo kingine siku ya Jumanne, bila ya kumtambua mtu huyo.
Hamas imesema imewaficha mateka hao katika “maeneo salama na vichuguu” huko Gaza, huku bibi mmoja aliyeachiliwa akisema alipelekwa chini ya ardhi kwenye “utando wa buibui” wa njia za kupita.