Nicholaus Mgaya(BOIMANDA) mkazi wa mji Mafinga mkoa wa Iringa amemuangukia Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb.) – Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuingilia kati mgogoro wa ardhi kati yake na baraza la waisilamu wilaya ya Mufindi (BAKWATA) kwa ardhi ambayo anadai aliinunua kwa Bw.Daniel Mahenge ambaye sasa ni marehemu mwaka 1998.
Akisimulia Mgaya alisema nilinunua eneo hilo hekari 20 wakati huo ikiwa ni kata ya Saohill,kijiji cha Changarawe ambapo sasa ni kata ya Changarawe na nilinunua kwa lengo la kujenga shule na chuo katika eneo hilo.
Baada ya kununua mwaka 2013 nilitaka kuendeleza kwa kufanya ujenzi kwenye eneo hilo lakini january mwaka 2014 uliibuka mgogoro ambapo BAKWATA wilaya walidai eneo hilo ni la kwao walipewa na raia wa Somalia aliyejulikana kwa jina la Mohamed Gahili ambapo kesi hiyo ilipelekwa baraza la ardhi la kata ya Saohill na baraza hilo lilimpa haki Mgaya kuwa mmiliki wa eneo hilo ambapo shahidi muhimu alikuwa mke wa marehemu Daniel Mahenge ambaye alithibitisha familia yake ilimuuzia Mgaya eneo hilo.
Boimanda anasema mpaka sasa bado kuna mvutano wa eneo hilo akiangukia serikali Rais Dr.Samia Suluhu Hassan kupitia kwa msaidizi wake waziri wa ardhi kumsaidia kupata haki yake ili kuendeleza eneo hilo ambalo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu akiamini serikali ni sikivu na ana imani haki yake itapatikana.