Ukarimu wa Nicki Minaj unaonekana hauna kikomo baada ya rapa huyo kujitolea kusaidia gharama za masomo za baadaye kwa kijana wa Chicago mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikamatwa na mama yake, Carlishia Hood, baada ya tukio la kupigwa risasi wiki kadhaa nyuma.
Hivi majuzi video iliibuka mtandaoni ambapo Hood alionekana akishambuliwa vikali na mwanamume anayeitwa Jeremy Brown wakati wa mabishano makali n wakati wa ghasia hizo,na kisha alimpiga risasi na kumuua Brown, ikisemekana kuwa ni katika juhudi za kumlinda mama yake.
Wawili hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka kuhusiana na kifo cha Brown hata hivyo, waendesha mashtaka wamewaondoa mashitaka hayo.
Siku ya Jumanne (Juni 27), Nicki Minaj alimtaja kijana huyo kwenye insta story yake , akimtaja kama “shujaa.”
Minaj alibainisha kuwa kijana huyo alifanya “kile ambacho mtoto yeyote angefanya.”
“Yule mvulana mwenye umri wa miaka 14 ambaye aliunga mkono tukio hilo wakati mtu mzima alipokuwa akimpiga mama yake usoni kana kwamba ni MWANAUME ni shujaa wa kweli,” aliandika. “Ikiwa anataka kwenda chuo kikuu, ningependa kusaidia. Ndivyo mtoto yeyote alipaswa kumfanyia mama yake. Alimlea mtoto wake vizuri na anapaswa kujivunia. Pia, Mungu alijua [kabla] alijua kwamba angeshambuliwa siku hiyo na kuhakikisha kwamba walikuwa na ulinzi kwenye Mungu ni MWEMA.”