Rapper kutokea kundi la Cash Money Records, Nicki Minaj amekuwa topic kubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya majibu yake kwa mtandao wa Bossip kuzua mjadala mkubwa siku chache zilizopita.
Mjadala huo ulianza siku mbili zilizopita baada ya mtandao wa Bossip kupost tweet kwenye page yao ya Twitter ikisema… “#seriousquestion kwanini hakuna wasanii wa kike wa hiphop wanaouza sana?”, tweet iliyoanzisha mjadala mkubwa na kuishia kuwataja wasanii kama Nicki Minaj ndani yake.
Watu wengi walioshiriki kwenye mjadala huo walisema wasanii wengi wa kike wanaofanya muziki wa Hiphop hawauzi kwa sababu hawana vipaji vitakavyoweza kuwaweka kwenye levo moja na wasanii wa kiume wa Hiphop… huku wengine wakimtolea mfano Nicki Minaj na kudai kuwa eti yeye hana kipaji wala mistari mizuri ila kinachofanya auze sana si muziki wake bali umbo lake!
Mjadala ukamfikia Nicki ambaye hakukaa kimya na kuamua kuwajibu ‘haters’ wote waliomshambulia haswa wale waliokuwa wanadai wanaume wengi hawajali kama mwanamke anajua kuimba au kurap ndio maana Nicki aliamua kuongeza umbo ili kuvutia biashara.
Hizi ni baadhi ya Tweets za Nicki Minaj nilizoweza kuzinasa:
>>> “Nimeenda mguu kwa mguu na kila MC wa kiume unayempenda. Kushusha uwezo wangu kama MC kwa levo hii kusema kweli ni kichekesho“. <<< @NickiMinaj.
>>> “Nimeona Bossip wana retweet ujinga kwahiyo nikaona ni bora niliachie. Lol. Wakubwa wananipa heshima yangu. Waandishi wakubwa pia“. <<< @NickiMinaj.
>>> “Kusema kuwa umbo la mtu ndio sababu wanapata feature za nyimbo na kuonyesha uwezo wao kwa kila MC mkali ambae yupo hai… (inasikitisha) Watu wesui bwana, badilikeni lol” <<< @NickiMinaj.
>>> “Lengo lenu kubwa maishani itakuwa ni kujaribu kuushusha uwezo wangu na mambo niliyofanya maishani. lol. Mtaisoma namba. Phaedra voice..” <<< @NickiMinaj.
>>> “Lol. Kwahiyo rappers wa kiume wanafanikiwa zaidi kwa sababu wana ….. kubwa?“<<< @NickiMinaj.
>>> “Kama rapper wa kiume angekuwa kwenye track moja na Wayne, Jay, Eminem, Kanye na wengine kwenye NGOMA juu ya NGOMA angetukuzwa kama MKALI pia. Wivu ni ugonjwa“. <<< @NickiMinaj.
>>> “Kutokunipa props zozote hainizuii mimi kuwa mkali. Mimi ni mogul. Chuki yenu ndiyo iliyofanya vyote hivi viwezekane. Lol. Asanteeeniii! Mmuuaahhh!!!” <<< @NickiMinaj.
Bossip nao hawakukaa kimya, hizi ni baadhi ya tweets zao nilizoweza kuzinasa:
>>> “Wow, swali letu limemfanya Nicki achemke kuliko hali ya hewa ya Africa Mashariki na Kati, violent…” <<<@Bossip.
>>> “Inakuaje hii issue imekuwa kuhusu watu weusi @NICKIMINAJ ???” <<< @Bossip.
>>> “Kwa namna moja ama nyingine swali letu dogo kuhusu marappers wa kike limegeuka kuwa topic kubwa kwa @NickiMinaj. Lazima uipende hii app…” <<< @Bossip.
>>> “Tumeshusha uwezo wako? Tutakuwa tulipitwa na hiyo sehemu…@NickiMinaj” <<< @Bossip.
Je, na wewe ni miongoni ya wale watu wanaoamini kuwa Nicki Minaj anauza zaidi kimuziki kwa sababu ya umbo lake?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE