Habari ya Asubuhi…! na karibu kwenye matangazo yetu hii leo 21.8.2023
Waaandamanaji hao wakiwa wanapeperusha bendera ya nchi yao, ile ya Urusi, China na India, walisikika wakiishtumu nchi ya Ufaransa iliyokuwa Koloni yake na kulaani vikwazo vya kiuchumi vilivyowekewa nchi yake na Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.
Aidha, waandamanaji hao walisikika wakisema hawaungi mkono mpango wa nchi za ECOWAS kuivamia nchi yao, ili kumrejesha rais Bazoum madarakani.
Maandamano hayo yamefanyika siku moja tu baada ya ujumbe wa ECOWAS ukiongozwa na aliyekuwa kiongozi wa kijeshi nchini Nigeria, Abdulsalami Abubakar kuzuru jijini Niamey kwa ajili ya mazungumzo.
Ujumbe huo ulikutana na uongozi kijeshi na rais Bazoum, huku kiongozi wa ujumbe huo akisema baada ya mazungumzo bado kuna tumaini la kupata mwafaka kwa njia ya mazungumzo.
Jumamosi iliyopita, kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdourahamane Tiani, alionya kuwa jaribio lolote la kuivamia Niger, halitakuwa rahisi na litakabiliwa kwa nguvu.
Aidha, Jenerali Tiani, aliahidi kurejesha madaraka kwa raia baada ya miaka mitatu.