Utawala wa kijeshi wa Niger ulitangaza Jumatatu kwamba umemaliza mashirikiano mawili ya kiusalama na ulinzi na Umoja wa Ulaya huku nchi hiyo ikitazama zaidi Urusi kwa ushirikiano wa kiulinzi.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ilisema taifa hilo linajiondoa katika Ujumbe wa Ushirikiano wa Kijeshi wa Umoja wa Ulaya (EUMPM) nchini Niger, na hivyo kubatilisha kibali cha mpango wa Umoja wa Ulaya ulioanzishwa ili kuongeza uwezo wa vikosi vya usalama vya nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Serikali imeamua “kuondoa marupurupu na kinga iliyotolewa” chini ya ujumbe wa ushirikiano wa kijeshi wa EU na kwa hiyo “haina wajibu wa kisheria” kuhusiana na ushirikiano huo, ilisema taarifa hiyo.
EUMPM ilizinduliwa mwezi Februari ili kuongeza uwezo wa Wanajeshi wa Niger kudhibiti vitisho vya kigaidi, kulingana na EU.
Junta pia ilibatilisha ujumbe wa 2012 wa kujenga uwezo wa raia wa EU ulioanzishwa ili kuimarisha vikosi vya usalama vya ndani vya nchi.