Serikali ya Nigeria imeishutumu kampuni ya China kwa kuanzisha kampeni ya kukamata mali zake nje ya nchi, zikiwemo ndege za rais, msemaji wa serikali alisema siku ya Alhamisi.
Msemaji wa Rais Bayo Onanuga alisema Zhongshan Fucheng Industrial Investment Co. Ltd. inatumia “njia zisizo za kawaida” kulenga mali ya serikali ya Nigeria, licha ya kutokuwa na majukumu ya kimkataba na serikali ya shirikisho.
Zhongshan hakujibu mara moja ombi la maoni.
Mzozo huo unatokana na mkataba wa mwaka 2007 kati ya Zhongshan na Jimbo la Ogun kusini magharibi mwa Nigeria kuunda eneo la biashara huria, ambalo lilikatishwa mwaka 2015.