Baada ya kutolewa kwenye hatua ya 16 bora ya kombe la dunia mabingwa wa Afrika Nigeria wapo hatarini kukumbwa na balaa lingine.
Mabingwa hao wa Afrika huenda wakapigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya soka baada ya mahakama nchini humo kutengua utawala wote ya shirikisho la soka nchini humo
Waziri wa michezo wa Nigeria Tammy Danagogo alimteua Lawrence Katiken kuwa msimamizi mkuu wa NFF.
Taarifa nchini humo zinasema kuwa matokeo duni ya timu hiyo hayakusaidia hali mbaya ya uhusiano na serikali ya nchi hiyo na shirikisho la soka.
Super Eagles iliambulia kichapo cha 2-0 mikononi mwa Ufaransa katika raundi ya pili ya kombe la dunia na hivyo kufungashwa virago.
Mahakama ya jimbo la Plateau ilitoa amri ya kupinga uongozi wa Aminu Maigari, na kamati yake nzima.
Kufuatia hatua hiyo Nigeria inaweza kuadhibiwa na FIFA ambayo inakataza mamlaka za kiserikali kuingilia mambo ya soka.