Nchini Nigeria, wanachama wa vyama vya wafanyakazi wanaandamana kupinga kupanda kwa bei ya mafuta na mfumuko wa bei unaosababishwa na kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta.:
Hii ni baada ya mazungumzo kati ya miungano hiyo na serikali kukosa kuafikia suluhu siku ya Jumanne.
Kiongozi wa muungano wa wafanyikazi nchini Nigeria Joe Ajaero aliwataka wanachama wake “kukusanyika katika majimbo yote nchini kote kutoa azimio hilo la pamoja”.
Mkuu wa polisi Kayode Egbetokun alionya dhidi ya ghasia wakati wa maandamano hayo na kuwataka maofisa wake kuwalinda waandamanaji.
Vyama vya wafanyakazi vimesema hatua zilizotangazwa na Rais Bola Tinubu siku ya Jumatatu ili kupunguza athari za kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta hazikutosha.
Serikali ilisema kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta kutasaidia kupunguza mzozo wa ufadhili wa serikali.