Serikali ya Nigeria imetangaza kuufungia mtandao wa Twitter nchini humo. Waziri wa Mawasiliano na Utamaduni, Lai Mohammed amesema uamuzi huo umetokana na kuwepo na kujirudia kwa matumizi ya mtandao huo katika kushusha hadhi ya nchi hiyo.
Uamuzi huu unakuja ikiwa ni siku moja baada ya Twitter kufuta tweets na video za Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari akitoa onyo la adhabu kwa kikundi cha IPOB akikishutumu kwa mashambulizi katika majengo ya Serikali. Twitter ilisema imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa tweet hizo zilikiuka kanuni za matumizi ya mtandao.
Sambamba na uamuzi huo, Serikali ya Nigeria imeiagiza Tume ya Taifa ya Utangazaji (NBC) kuanza mchakato wa kutoa leseni kwa mitandao yote ya kijamii inayotoa huduma ya kurusha video nchini humo.
MSITU WA SHETANI, NGUVU ZA GIZA, MAAJABU YA KUTISHA, KONDOO 2OO NA WATU WAMEMEZWA