Aliyekuwa mfanyakazi wa Bodi ya Elimu ya Msingi kwa Wote ya Jimbo la Adamawa, Aminu Mahdi amekamatwa kwa madai ya kumpiga mkewe hadi kumuua.
Aminu mwenye umri wa miaka 63 anayetokea katika Kata ya Yelwa katika eneo la serikali ya mtaa wa Mubi Kaskazini mwa Nigeria anadaiwa kumshambulia mke wake wa pili Hadiza Zubuchi (46) kwa kumnyima kulala nae kitandani.
Mtuhumiwa huyo ambaye amekiri kutenda kosa hilo, aliwaambia polisi kuwa hakukusudia mke wake afe, kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa Polisi wa jimbo hilo, SP Suleiman Nguroje.
Nguroje alifichua katika mazungumzo na wanahabari siku ya Alhamisi kwamba Aminu alirejea nyumbani saa 9:00 alasiri Jumapili iliyopita, Agosti 27, 2023, ili na kudai haki ya ndoa na kusababisha mabishano ambayo yalifikia kilele cha kumfukuza mkewe.
Nguroje alisema baada ya Aminu kula chakula na kubadilisha nguo, alikwenda chumbani alikokuwa alale na mkewe, lakini mkewe alimnyima matumizi ya kitanda chake.
Kwa vile mke hakumruhusu amguse na badala yake akaanza kumpiga kwa fimbo, alimpokonya fimbo hiyo na kumpiga mara kwa mara.
Kulingana na Daily post inasemekana kuwa kipigo hicho kilikuwa kikali sana hivi kwamba mke, ambaye alimuoa mnamo 2016, alikufa hatimaye.
Kwa majuto alipokuwa akiwaeleza polisi hadithi yake, Aminu alisema, “Sikutarajia kwamba tukio la aina hii lingenipata. Lilikuwa kosa.”