Rais Samia Suluhu Hassan, “Nchi ipo kwenye mikono salama, Mimi na mwenzangu, Dk. Hussein Mwinyi tutahakikisha inafika pale ambapo Rais Magufuli alitaka kuifikisha…
“Dk Magufuli ameondoka mapema lakini ameshafanya kazi ambayo alikuja kuifanya Duniani, kazi ambayo ni kuonesha njia, nasi hatuna budi kuifuata,” amesema Rais Samia.
“Ni siku nyingine ngumu katika historia ya nchi yetu, tarehe 17 ilikuwa ni siku ngumu nilipotakiwa kutangaza kifo cha Rais haikuwa rahisi nilihisi nafanya makosa kumtangaza Rais wangu amefariki, lakini nikaambiwa hakuna wa kutangaza isipokuwa wewe,” Rais Samia
“Hayati Rais Magufuli alijikita kujenga uchumi wa ndani unaotegemea rasilimali za ndani, na kuziba mianya ya rushwa, alijikita kufufua na kujenga miradi ya kimkakati, azma ya Magufuli ilikuwa ni Tanzania ya viwanda, ambayo aliamini bila viwanda uchumi wa Tanzania itakuwa ndoto,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu