Isabella Mwampamba ni Mtanzania wa kwanza kuripotiwa kuwa ana virusi vya corona Tanzania, leo amekubali kuzungumza kuhusu jinsi alivyopata maambukizi, jinsi Watu wanavyomchukulia mtaani na zaidi anasema kilichomuumiza ni pale Watu walipokuwa wanadai ametumwa kuleta corona na ikiwezekana auawe.
“Niliumia sana Watanzania walipokuwa wanaandika mitandaoni huyu Mtu ametumwa, ametumiwa kuleta ugonjwa, wengine wakawa wanasema achomwe sindano auawe, nikapata taharuki, mwingine akaniambia ungekuwa mjini ungekatwa mapanga” – Isabella