Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amemuagiza Injinia wa ujenzi Wilayani humo kuhakikisha anarejesha gharama zote za milango na fedha zilizotumika vibaya kutokana na usimamizi wake mbovu wa ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Shule ya Chekereni Wilayani humo.
Lengai Ole Sabaya awali aliamuru gharama hizo zilipwe wakiwa chini ya ulinzi maelekezo aliyoyatengua muda mfupi baada ya Injinia huyo kukiri kufanya makosa na kuomba siku 7 kulipa fidia ya upotevu na ubadhilifu huo.