Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua, ambaye anakabiliwa na uwezekano wa kushtakiwa, amesema atajitetea mbele ya Bunge la Kitaifa la nchi hiyo siku ya leo Jumanne.
Gachagua, ambaye alihutubia taifa kutoka katika makazi yake rasmi katika mji mkuu Nairobi siku ya Jumatatu, alisema atajitolea “kupatikana ili kushtaki utetezi wangu kwa saa mbili.”
Bunge la Kitaifa, lenye wajumbe 349, litasikiliza utetezi wa Gachagua na baadaye kupiga kura ya kumshtaki au la.
Angalau theluthi mbili ya wanachama – sawa na 233 – wanahitaji kupiga kura kuunga mkono kushtakiwa kwake, ili uamuzi huo upelekwe kwa Seneti.
Bunge la Seneti lenye wanachama 67 pia litasikiliza mashtaka hayo, na ikiwa zaidi ya theluthi mbili – au wanachama 45 – watapiga kura kumshtaki Gachagua, naibu rais ataacha kushikilia wadhifa huo.
Miongoni mwa sababu nyingine, Gachagua anatuhumiwa kujipatia utajiri wa thamani ya shilingi bilioni 5.2 za Kenya, au dola milioni 40.3, kinyume cha sheria katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Mwengi Mutuse, mwasilishaji wa hoja ya kumtimua Gachagua, anasema katika miaka miwili iliyopita, naibu wa rais alipokea mshahara wa shilingi milioni 24, au dola 186,000.
Mutuse aliongeza kuwa katika maandalizi ya uchaguzi wa urais wa Agosti 2022, Gachagua alitangaza utajiri wake kuwa shilingi milioni 800, au dola milioni 6.8.