Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa limesema kwamba idadi ya Watu walio hatarini kutumbukia kwenye baa la njaa katika Mataifa 43 imeongezeka hadi Milioni 45, wakati njaa ikiongezeka kote ulimwenguni.
Shirika hilo la WFP limesema kwamba idadi hiyo iliyokuwa Milioni 42 mwanzoni mwa mwaka, imeongezeka kutokana na Watu wengine Milioni tatu wanaokabiliwa na njaa nchini Afghanistan.
Mkurugenzi Mtendaji wa WFP David Beasley amesema sababu kuu za ongezeko hilo ni mizozo, athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na njanga la COVID-19.
WFP imesema gharama ya kuepusha njaa duniani inafikia Dola Bilioni saba, kutoka Dola Bilioni 6.6 iliyokadiriwa mwanzoni mwa mwaka, WFM imesema ufadhili uliozoeleka hautatosha tena.