Hadi Machi 12, 2020 jumla ya visa vya Virusi vya Corona vilivyoripotiwa duniani kote ni zaidi ya 129,000 ambapo vifo ni 4,749 na watu waliopona wakiwa ni zaidi ya 68,667.
Virusi hivi vimezidi kusambaa kwa kasi duniani kutokana na urahisi wake wa kuenea ambapo mtu aliyeathirika anaweza kumuambukiza mwenzake akikohoa au kupumua na kurusha matone ya mate ambayo yanakuwa na virusi hivyo.
Katika maeneo ya kazi, mate hayo yakidondoka kwenye meza, laptop, tablets na ukiyagusa kwa mikono na kisha ukagusa uso wako (macho, pua, mdomo), maambukizi yanaenea zaidi.
Kutokana na hatari hiyo, hizi ni njia sita rahisi za kujikinga virusi hivyo;