Imeelezwa kuwa ili kuepuka athari za mikopo chechefu ni vyema wananchi wakatumia taasisi rasmi za kifedha pamoja na vyama vya ushirika katika kukopa hali itakayosaidia kulinda mitaji ya biashara zao na hatimaye kuchagiza maendeo endelevu katika jamii.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Ngome Kanali Aisha Matanza kwenye semina na mafunzo ya siku tatu kwa wawakilishi wa chama cha hiko ambapo amesema mpaka sasa chama hiko kina zaidi ya wanachama 15,000 na mtaji wa zaidi ya shilingi Bilioni 50 unaosaidi kutoa masuluhisho ya kifedha kwa changamoto mbalimbali za wanachama.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu Meja Jenerali Fadhili Nondo amewaas wanachama hao kutumia mafunzo watakayoyapata kujiongezea ujuzi wa masuala ya ushirika ili kuleta tija iliyokusudiwa katika kukuza vitapo vyao na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao baadi ya wanachama wa chama hiko akiwemo Luteni Kanali Cleopatra Calistus pamoja na pamoja na Badi Shabani kutoka makao makuu ya Jeshi Dodoma wameeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia katika kuimarisha mitaji yao na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi.