Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Saidi Mtanda ametekeleza agizo la Rais Magufuli na kukabidhi fedha kwa Mama aliyelalamika kuibiwa ng’ombe mbele ya JPM, DC Mtanda amemkabidhi fedha hizo Mwanamke huyo mbele ya wenzake ambao kwa pamoja wanawamiliki ng’ombe hao na amewasainisha nmkataba ili kuepuka mkanganyiko hapo baadae.
Rais Magufuli juzi alitoa siku 5 kwa DC Mtanda na RPC wa Rukwa kuhakikisha wanamlipa Tsh.Milllion 15 kama hela ya fidia na usumbufu Mwanamke huyo aliyelalamika kuibiwa ng’ombe wake 25, kufuatia mtuhumiwa aliyekiri kufanya wizi huo kukimbia baada ya kupewa dhamana ya Polisi.
“Hapa Rais Magufuli ametuhurumia na hii anatuonesha alarm kwamba tukishindwa kufanya hivi tunaweza kupata madhara makubwa, sio ya kulipa fedha tu, tunaweza hata kufukuzwa kazi au kujiuzulu, tuwe waangalifu tufanye kazi kwa mategemeo yale ya Rais”– DC MTANDA
KESI YA BILIONI 309 ZA ESCROW: SETH WA IPTL, RUGEMALIRA WAMWANGUKIA DPP