Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi Nyumba ya kuishi madaktari wawili wa zahanati ya Kizimkazi Wilaya Ya Kusini Unguja, Zanzibar mradi ambao umedhaminiwa na SportPesa.
Jengo lilianziwa ukarabati rasmi mwezi February 2018 baada ya wafadhili SportPesa kutembelea na kuona maendeleo ya jengo hilo kuwa katika hali mbaya na halikuwa salama kwa daktari anayehusika kusimamia na kuokoa maisha ya watu.
Kwa upande wa Daktari wa zahanati ya Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja Bi Suleha Nuhuu ambaye ndiye ataitumia nyumba hiyo kama makazi ameshukuru uongozi wa SportPesa kwa kukamilisha umalizikaji wa jengo hilo na kwa juhudi walizozionyesha kwa kukamilisha jengo wa wakati.
Uzinduzi huo ambao ulifanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ulihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo mkurugenzi wa utawala na utekelezaji wa kampuni ya michezo ya kubashiri Abbas Tarimba.
Haji Manara haishiwi maneno “Kabla ya kunitolea povu nipinge kwa data”