Taarifa ikufikie kuwa Benki yako ya Nmb imetoa udhamini wa shilingi Milioni 75 kuwezesha kufanikisha mkutano wa Makamanda mbalimbali wa Jeshi la Polisi Tanzania unaodumu kwa muda wa wiki moja.
Mkutano unajumuisha makamishna,Makamanda wa Mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani na ni mkutano mkuu wa 6 wa maafisa wa jeshi la polisi nchini ambao bado unaendelea katika chuo cha taaluma ya jeshi la Moshi (MPA) Mkoani Kilimanjaro.
Mbali na Makamishina na Makamanda wa Polisi wa Bara na Visiwani Mkutani huu pia umejumuisha pia na maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao makuu na ulizinduliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Pereira Sirima.
Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini Bi. Vicky Bishubo amesema udhamini huo unajumuisha usafiri wa mabasi kwa washiriki wote kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani pamoja na maandalizi ya mkutano huo.
Pamoja na hayo NMB pia imetoa Kompyuta mpakato{Laptop} nne zitakazowezesha mipango ya Jeshi ya kupambana na Uhalifu wa Mitandao,Mikoba,Notebook na kalamu za kutosha.