Leo July 3,2018 nakusogezea stori kutoka huko nchini Pakistan ambapo unaambiwa kuwa Mwanasiasa mmoja nchini Pakistan amewashangaza wengi kwa tabia yake ya kufanyia kampeni zake za kisiasa jalalani na kwenye mifereji ya maji machafu.
Mwanasiasa huyo anayejulikana kama Ayaz Memon Motiwala ameonekana katika eneo la Karachi nchini humo akipiga kampeni zake jalalani na hakuishia hapo tu bali alienda na kwenye mifereji ya maji machafu na kukaa chini huku akinywa maji hayo machafu na kuwaomba Wananchi wa eneo hilo wampigie kura katika uchaguzi unaokuja.
Inadaiwa kuwa Mr. Motiwala yeye ni mgombea binafsi na ana itaka kwa udi na uvumba nafasi anayogombea na ndio maana anafanya hivyo ili kuwashawishi Watu wampigie kura.
Aidha nchi ya Pakistan inategemea kufanya uchaguzi mkuu July 25 mwaka huu.